Kwa Wasomaji wa Kiswahili

SHEN Du / 沈度 (1414)  GiraffePainting / 瑞应麒麟图

Shen Du / 沈度 (1414) Mchoro wa Twiga / 瑞应麒麟图

Shen Yuning (沈玉宁) ni mhariri wa Kamusi Mpya ya Kiswahili-Kichina (Toleo kwenye Intaneti). Hivi sasa anashughulikia sana kuendeleza mradi wake wa shahada ya uzamifu huko chuo kikuu cha Hamburg. Mada yake iko chini ya isimu-historia ya kibantu.

Mwishoni mwa mwaka wa 2011 mradi huu wa kutengeneza kamusi ya Kiswahili-Kichina (Swahili-Chinese Dictionary Project kwa lugha ya Kiingereza) ulianzishwa kama jitihada binafsi ya mhariri inayolenga utafsiri wa ujuzi (tovuti kwa lugha ya Kiingereza, pia haipatikani tena). Mwanzoni mradi huu ulipata ufadhili wake wote kupitia mchango wa maandishi (grant writing) kutoka mtandao wa kijamii wa weibo.com kwa muda wa mwaka mmoja na nusu na baadaye kutoka rafiki wa karibu wa mhariri. Kwa bahati mbaya hii kazi haikupata nafasi ya kuchapishwa nchini Uchina. Katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2014 mhariri aliamua kuweka maneno mengi ya msingi kwenye mtandao kwa sababu ya ukosefu wa ufadhili wakati huo.

Anwani ya barua pepe:
     ynshen[at]outlook.com
     habari[at]siwaxili.com
Twitter:
     @ShenYuning